'kushughulikia mfumo wa ikolojia'
Wawindaji wamerejesha mamia ya ardhi ya chemichemi katika Amerika Kaskazini kwa usaidizi kutoka © Ducks Unlimited
Kushughulikia mfumo wa ikolojia kunakubali kwamba mabadiliko katika mfumo wa ikolojia na viumbe vyao hayawezi kuepukwa kwa sababu ya michakato ya kiasili, inayoweza kuwa haraka au polepole. Kwa mfano, maziwa yasiyo na vina hujazwa na uchafu kutoka milimani. Binadamu hubadilisha mifumo ya ikolojia kwa makusudi, kwa mfano kubadilisha misitu kuwa mashamba, na bila kujua wakati mashamba yaliyolimwa sana huoshwa na kuwa jangwa au kupunguza manufaa na kuwa ardhi kame. Shughuli nyingine za binadamu bila kumaanisha huharakisha mabadiliko asili, kama vile kupitia mabadiliko ya mazingira. Shughuli za binadamu kwa mfumo wa ikolojia wakati mwingine zinaweza kupunguzwa kwa urahisi, iwapo wanaotumia mazao haya ya mifumo ya ikolojia watachukua jukumu. Kwa hivyo, wavuvi waendeleze matumizi ya ngazi za samaki katika mabwawa na wawindaji wa bata warejeshe ardhi chemichemi. Uharibifu kwa mazingira unawezwa kurekebishwa kwa haraka iwapo elimu muhimu inasaidia kuendeleza ujuzi mashinani na kuna pesa za kutosha kusawazisha juhudi za jamii za mashinani, zikiongozwa na jamii husika.
Viumbe mwitu kuzoea mabadiliko
Kuzaana kwa mbayuwayu kumehamia kaskazini © Gallinago_media/Shutterstock
Kasi ya mabadiliko ya mfumo wa ikolojia imeonyeshwa na sehemu ya vumbe vyake. Nje ya tropiki,maua yanastawi na wadudu hutokea mapema kila mwaka kwa sababu ya kupanda kwa viwango vya joto. Katika tropiki, mabadiliko ya mvua yanaathiri mimea. Mienendo hii miwili inaweza kuonekana kwa wakati na kupata makao kwa ndege wa kuhamahama, wengine wakihamia kithabiti kaskazini ili kuzaana. Viumbe wanaotulia pahali pamoja kwa muda wakati mwingine huzoea vizuri, lakini hawawezi kutawanyika haraka kuenda sehemu ngeni, haswa iwapo wamezuiwa na pwani au katika milima iliyo kivyake. Kila kiumbe hula na huliwa , kwa hivyo kutoweka mtaani kwa kiumbe kimoja kunaathiri vingine katika mfumo wa ikolojia huo pia. Kila mtu anahitaji kujua kuhusu mabadiliko makubwa dhahiri yanayotokea katika sayari yao,na kinachomaanisha kwao na familia zao. Shule yako mtaani au pahali pa kazi ni kituo cha rekodi kama hizi?
Kuzoea kwa binadamu
Ng'ombe watamu walizoea misitu katika Kolombia © April DeBord/Shutterstock
Hata wanaoishi mijini hutegemea mifumo ya ikolojia kwa chakula, maji na hewa, kwa hivyo mabadiliko hutuathiri sote. Wakulima wa kilimo wAnahitaji hali ya hewa inayotabirika kwa urahisi kupanda mimea kila mwaka. Kuna mabadiliko zaidi jinsi nyasi ya mifugo inamea, katika malisho yenye ubaridi au katika vilima kavu, na uwingi wa uhifadhi kukabiliana na ukuwaji mbaya wa muda mfupi. Hata hivyo, kutokuwepo kwa mvua kwa muda mrefu ni shida kwa mimea na mifugo, na kuzuia moto misituni wakati wote kwa miaka mingi ya ukuzi kwa minajili ya mbao. Kwa bahati nzuri, misitu inaweza kusaidia kuhifadhi unyevunyevu mchangani, vile vile kufungia kaboni, na binadamu kupunguza kula nyama kutoka mashambani itapunguza utoaji wa gesi chafu kutoka kwa mifugo. Hata hivyo, ulaji wa nyama unaweza kuwa njia bora zaidi ya matumizi ya mchanga kwa muda mrefu na ardhi isiyofaa kwa upanzi wa mimea. Kutumia viumbe mwitu kunaweza kustawisha kuliko mifugo katika ardhi kama hii, inavyopatikana katika sehemu za Kiafrika ambako gharama ya kuzuia magonjwa katika wanyama iko juu, na hali hiyo hiyo katika sehemu zinginezo zilizobadilishwa kuwa mwitu. Mazingira tajiri katika ardhi kama hii inaweza kuongeza bidii ya kimaisha huku hali ya hewa ikibadilika. Ni muhimu haswa kuhifadhi elimu ya kitamaduni ili kuhifadhi sehemu kama hizi. ambayo mara nyingi imepotezwa kwa sababu ardhi imebadilishwa kufaa sana kilimo cha mashine.